Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAUGUZI MUHIMBILI WAADHIMISHA SIKU YAO LEO

  Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akisoma kiapo kwa wauguzi katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika hospitali hiyo. 
 Wauguzi wa hospitali hiyo wakila kiapo katika maazimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.

 Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sabastian Luziga. 

PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

KAIMU  Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amewakumbusha wauguzi kufanya kazi kwa kufuata maadili na misingi ya taaluma yao na kuwafichua wachache ambao wanaenda kinyume na maadili kazi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Profesa Museru ametoa wito huo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duaniani , ambapo wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo wameadhimisha siku hiyo.

Katika maadhimisho hayo Profesa Museru amewasisitiza wauguzi hao kutambua kwamba muuguzi ni mtu muhimu katika kutoa huduma, hivyo hawana budi kuwahudumia wagonjwa kwa moyo ili kuondoa malalamiko.

“ Nawaomba muwafichue wale wachache ambao wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa kwani mkifanya hivyo mtatusaidia sana kuondoa kero na malalamiko yanayotolewa dhidi yenu,” amesema Profesa Museru.

Mipango ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akielezea mipango ya MNH Profesa Museru amesema Hospitali hiyo ina mpango wa kuwaendeleza kitaaluma watumishi wake wakiwemo wauguzi ili watoe huduma yenye kiwango cha juu zaidi.
Mpango mwingine ni kuboresha sehemu za kufanyia kazi, kununua vifaa tiba kadiri fedha zinavyopatikana pamoja na kutafuta kibali kwa lengo la kuajiri wauguzi wengine ili wasaidie kutoa huduma kwani wauguzi waliopo sasa hawatoshelezi mahitaji.

Kutekeleza agizo la Rais
Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya mabadiliko makubwa katika kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli na kuhakikisha kwamba wagonjwa wanaokuja kutibiwa MNH wanapata dawa na kupata vipimo kwa wakati. 

Hivyo ametoa wito kwa wauguzi kushiriki katika jitihada zote zinazofanywa na Hospitali katika kuongeza mapato ya hospitali hiyo.

Akisoma risala ya wauguzi, Mwenyekeiti wa chama cha wauguzi Tawi la MNH, Sebastian Luziga amesema changamoto inayowakabili ni kuwapo kwa idadi ndogo ya wauguzi hali inayoathiri utendaji kazi.


“Idadi ya wauguzi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wagonjwa kwani kwa siku muuguzi anahudumia wagonjwa kati ya 20 hadi 30 tofauti na uwiano ambao muuguzi mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa 6 hadi 8 kwa siku.” Amesema Sebastian.

Kauli mbiu ya siku ya wauguzi Duniani mwaka huu ni “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko, Uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”


Mei 12 wauguzi wote Duniani wanamkumbuka muasisi wa uuguzi mama Florence Ningtngale.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top