Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI NCHEMBA ATUMBUA MAJIPU JIMBONI KWAKE ... AVUNJA BODI YA MAJI BAADA YA KUGUNDUA UFISADI WA MAMILIONI

WAZIRI wa Kilimo Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ajitolea kulipia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa kusaidia matengenezo ya mashine ya maji huku akitumbua majipu kwa kuwasimamisha kazi viongozi 15 bodi ya maji ya kijiji cha Mingela jimboni kwake Iramba wilaya ya Iramba mkoani Singida baada ya bodi hiyo kufanya ufisadi wa milioni 9 za mradi wa maji wa kijiji hicho.

Viongozi hao ambao ni pamoja na afisamtendaji wa kijiji cha Mingela ,Mwenyekiti ,katibu ,mhasibu na wajumbe 12 ambao walikuwa wakiunda bodi hiyo ya maji waliwasimamisha baada ya kutafuna pesa hizo za mradi wa maji na kushindwa kulipia milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya mashine iliyoharibika . 

Nchemba ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba alifikia uamuzi huo wa kuivunja bodi hiyo ya maji kijijini hapo jana baada ya wananchi wa kijiji hicho kulalamika katika mkutano wake wa hadhara kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumchagua na kuanza kutimiza sehemu ya ahadi zake ,kuwa hawana huduma ya maji safi baada kukosa Tsh milioni 2 za kutengeneza mashine ya maji iliyoharibika kwa muda sasa.

Kutokana na kilio hicho cha wananchi Nchemba alilazimika kumwita jukwaani afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Said Mussa na bodi yake ili kueleza mapato na matumizi ya mradi huo wa maji yapo kiasi gani na yapo wapi ,swali lililopelekea viongozi hao kujichanganya kujibu kuwa ni kweli makusanyo ya mradi huo wa maji ni zaidi ya Tsh milioni 9.4 ila benki zipo kiasi cha Tsh 400,000 na pesa nyingine zimetumika kukarabati mashine hiyo iliyokuwa ikihitaji kutengenezwa kwa Tsh milioni 2 .
Waziri wa kilimo , mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akipokelewa na wananchi wa kata ya Tulia jimboni kwake Iramba jana 
Waziri Mwigulu akilakiwa na wapiga kura wake wakati wa mikutano yake ya kuwashukuru 
Waziri Nchemba akiwapungia mikono wananchi wake 
waziri Nchemba akiteta jambo na mmoja kati ya walemavu katika kata ya Tulia jimboni Iramba .
Waziri wa kilimo ,chakula na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi wa bodi ya maji Mingela Iramba kwa ufisadi wa mamilioni ya maji 
Waziri Nchemba akiwa na mmoja kati ya walemavu wa ngozi katika jimboni kwake 


Na Matukiodaima Blog 
Mganganyiko huu ulimlazimu waziri huyo kuivunja bodi hiyo ya maji na kumwagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Clement Berege kupeleka wakaguzi wa ndani mara moja katika kijiji hicho ili kukagua mapato na matumizi pamoja na kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi huo wa pesa za makusanyo ya maji.

Alisema kuwa ni ufisadi mkubwa ambao umefanywa na viongozi hao wa bodi ya maji katika kijiji hicho kwa kutafuna pesa zote pasipo matengemnezo ya mashine ya maradi huo wa maji."Yaani ni ufisadi mtupu ambao sikubaliani nao hata kidogo mashine ya kutengenezwa milioni 2 imetengenezwa kwa milioni 9 na bado haifanyi kazi .....naomba wote mliohusika na ufisadi huu kuanzia leo mkae pembeni na wakabidhiwe ofisi watu wengine ......pia mkurugenzi kuanzia sasa vitabu vyote vya makusanyo ya mapato vithibitiwe ili kuepusha kupoteza ushahidi " 

Hata hivyo aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kutuma wakaguzi wa ndani katika vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ili kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi kwenye vijiji vyote .Alisema yawezekana viongozi wa vijiji wamekuwa wakitumia vibaya makusanyo ya pesa za wananchi bila kufuata utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa taratibu.

Katika hatua nyingine Bw Nchemba aliutaka uongozi wa serikali za vijiji katika wilaya hiyo ya Iramba kuacha kuendelea kuwatoza wananchi ushuru kandamizi wa biashara ndogo ndogo hasa zile zilizopigwa marufuku wakati wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoza ushuru wa Tsh 10,000 kwa biashara ambayo mwananchi akiuza yote faida yake anaambulia Tsh 5000 hivyo alishauri uongozi wa Halmashauri kushusha ushuru huo ambao ulikuwa maalum kwa mapambano ya ugonjwa wa kipindupindu na kuwatoza ushuru wa Tsh 3500 kwa wananchi wanaojishughulisha kufanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo ya upikaji pombe kwa ajili ya kuendesha maisha yao. 

Pia alitaka wananchi kuendelea kudumisha usafi katika biashara zao ili kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu ,kwa wananchi ambao walipatwa na maafa wakati wa mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu ,alisema kuwa wataalam wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu watafika kufanya tathimini ili kuwasaidia wananchi hao.

Akijibu tuhuma hizo mbele ya waziri Nchemba afisa mtendaji wa kijiji cha Mingella Bw Said Mussa alisema kuwa ni kweli walikusanya milioni 9.4 za mradi huo wa maji na fundi kutoka mjini Iramba anahitaji milioni 2 kwa ajili ya kutengeneza mashine hiyo ila kiasi cha pesa kilichopo benki ya Tsh 400,000 pekee hivyo hawana uwezo wa kulipia gharama za fundi.Alisema kuwa kwa upande wake hajui mhusika halisi wa ufisadi huo lakini kwa kuwa waziri amesimamisha kazi wote basi itasaidia kumpata mhusika. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top