Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZAWADI YA MSHINDI WA MISS DAR CITY CENTRE YATANGAZWA

1.Mratibu wa Mashindano ya Miss Dar City Centre.....(katikati) akisoma taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani.
Mratibu wa shindano hilo la Miss Dar City Centre, Nancy Joseph (katikati) akisoma taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
2.Baadhi ya washiriki wa Miss Dar City Centre wakiwa nyuma ya mratibu wa mashindano hayo.
Baadhi ya washiriki wa Miss Dar City Centre wakiwa nyuma ya mratibu wa shindano hilo.
3
Washiriki hao wakisoma habari mbalimbali zilizoandikwa ndani ya Gazeti la Amani.
4. Washiriki hao wakisoma habari mbalimbali zilizoandikwa ndani ya Gazeti la Amani.5.Washiriki wa urembo Miss Dar City Centre wakisoma Gazeti la Amani.
Washiriki wa Miss Dar City Centre wakiendelea kusoma Gazeti la Amani.
ZIKIWA zimesalia siku mbili kabla ya kufanyika kwa shindano kubwa la warembo lijulikanalo kama Zan Aqua Miss Dar City Centre ndani ya Ukumbi wa Mtana (Jengo la LAPF) Kijitonyama jijini Dar mshindi wa kwanza Miss Dar City Centre atajinyakulia shilingi milioni mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph alisema kuwa, milioni hizo mbili atakazokabidhiwa mshindi wa kwanza, milioni moja itakuwa taslimu na milioni moja nyingine itakuwa ni thamani ya nywele bandia kutoka katika kampuni ya Prima Afro.
“Mbali na mshindi wa kwanza kumzawadia milioni mbili, mshindi wa pili atapewa milioni moja na laki tano itakuwa thamani ya nywele bandia, wa tatu laki nne na laki mbili thamani ya nywele bandia, wa nne na tano watapata fedha taslimu laki moja moja,” alisema Nancy.
Shindano hilo limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.
Na Denis Mtima/GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top