Wakati wapinzani wao wakuu katika huduma za ujumbe mfupi wa maneno (Instant Messengers) Whatsapp wakisuasua kuachia huduma ya simu za video, BBM wameachia huduma hiyo.
Kadri siku zinavyozidi kwenda kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia inashika moto kwa makampuni pinzani kuonyeshana umwamba katika ubunifu wa bidhaa bora na za kisasa zaidi.
Wakati Skype na Imo wakiwa wametawala soko la simu za video kupitia mtandao, Blackberry wameamua kuja na huduma hiyo mwaka huu huku ikionekana kupendwa zaidi na watumiaji wake.
Blackberry kupitia huduma yao ya BBM (Blackberry Messenger) wameamua kujua na huduma ya kupiga simu za video kwa mataifa yote sasa. hapo awali walianza kuachia huduma hiyo kwa mataifa ya Canada na Marekani.
Huduma ya simu za video itapatikana kwa watumiaji wa BBM wa iOS, Android pamoja na Blackberry. Hata hivyo huduma hiyo ipo kwenye toleo la majaribio (beta version) hivyo inatarajiwa kuwa na baadhi ya mapungufu.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
Magazeti ya leo Aprili 26, 20241 hour ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment