Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MEYA KINONDONI AAGIZA WATU KUBOMOA NYUMBA ZAO KWA HIARI


Mstaiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob amesema wananchi wote ambao wamewekewa alama za X kwenye nyumba zao na hawana mlalamiko yoyote ambayo yanafahamika kisheria na mahakama, wabomoe nyumba zao kwa hiari yao.

‘’Mtu akiwekewa alama ya X anatakiwa ndani ya siku 14 kama ana malalamiko yoyote aweze kupeleka mahakamani kwa ajili ya kuweka zuio na hili litafanikiwa kama ana hati ya nyumba na vielelezo vyote vinavyohitajika kisheria’’-Amesema Mstahiki Meya.

Aidha Meya amesema kwamba kwa nyumba zote ambazo zipo katika maeneo ya wazi na ambayo yabebainishwa kisheria kama maeneo ya umma na kuwekewa X nyumba hizo zitabomolewa muda sii mrefu baada ya kukamilika kwa kijiko cha kubomoa ambacho kilikuwa kimeharibika.

Hata hivyo Meya amesema watu wote waliowekewa X maeneo yote ya maskini na matajiri yatabomolewa nyumba zao hivyo hakuna mtu ambaye atakuwa juu ya sheria.

Kwa upande mwingine Meya amewataka wananchi ambao wamebomolewa nyumba zao maeneo ya mabondeni na wameanza kurejea watambue bado serikali ipo na itawaondoa hivyo ni bora watafute utaratibu mwingine.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top