Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RATIBA YA EURO 2016 HATUA YA 16 BORA YATOKA ... HII HAPA

Baada ya mechi za makundi kumalizika jana, sasa inafuata hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016. Ni baada ya mechi kali na za kusisimua zilizoshuhudia Ureno na Ireland zikipenya dakika za mwisho .

Kuna mechi kadhaa ambazo zinaturudisha kwenye historia ya mashindano haya na zinatarajia kuwa na presha kubwa kuanzia kwa wachezaji, mabenchi ya ufundi na hata mashabiki pia.

Italy v Spain inatarajiwa kuwa mechi kali mchezo ambao unazirejesha timu hizo kwenye kumbukumbu ya mchezo wa fainali ya Euro 2012 ambao Spain walishinda kwa bao 4-0.

Spain pia iliifunga Italy kwenye michuano ya Euro 2008, kwa hiyo Italy vichwani mwao watakuwa na kibarua cha kulipa kisasi watakapokutana siku ya Jumatatu.

Ufaransa v Ireland ni game nyingine ianayotazamwa kwa uzito wa aina yake licha ya Ireland kuonekana kama vibonde mbele ya Ufaransa. Goli la mkono la Thierry Henry bado linawakumbusha machungu Ireland pale waliposhindwa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia.

Ratiba kamili ipo kama ifuatavyo:

Switzerland v Poland (Jumamosi)

Wales v Northern Ireland (Jumamosi)

Croatia v Portugal (Jumamosi)

France v Republic of Ireland (Jumapili)

Germany v Slovakia (Jumapili)

Hungary v Belgium (Jumapili)

Italy v Spain (Jumatatu)

England v Iceland (Jumatatu)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top