Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA TSH. BILIONI 440


Na Eliphace Marwa-Maelezo
Benki ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kifedha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa huduma za msingi za kijamii nchini kupitia miradi mbalimbali iliyo chini ya Benki hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms. Bella Bird wakati wa kusaini hati ya makubaliano kuwa kutokana na umuhimu wa kusaidia kaya maskini kupitia mradi wa TASAF, Benki ya Dunia imetoa kiasi cha Dola za Kimarekani 200 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 440.

“Ili Tanzania iweze kupambana na umaskini inahitaji kuhakikisha kaya maskini zinapata huduma bora za afya na elimu ili kuweza kutimiza malengo yake, Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kifedha ili kufikia malengo yaliyoainishwa na serikali,” amesema Ms. Bella Bird.

Aidha Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa kupambana na umaskini katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kuleta maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa katika kipindi cha miaka hamsini ya ushirikiano na benki ya Dunia katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikali imeshuhudia mchango mkubwa wa kifedha na kitaalam toka Benki ya Dunia.

“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wake mkubwa wa kitaalam na kifedha kwani mpaka sasa Serikali iko katika majadiliano na Benki ya Dunia ili kuboresha bandari yetu ya Dar es Salaam,” amesema Dkt. Dkt. Likwelile.

Aidha Dkt. Likwelile amezitaka Taasisi zote zinazopata fedha kutoka Benki ya Dunia zitumie fedha hizo vizuri ili ziweze kuwanufaisha walengwa na kuleta tija kwa Taifa.

Benki ya Dunia inaisaidia Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia miradi yake mbalimbali ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini hapa nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top