Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WALIOCHANGANYA MAITI MUHIMBILI WATUMBULIWA ... UTEUZI MPYA WAFANYIKA

Dar  es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk Praxeda Ogweyo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kutokana na  kushindwa kusimamia vizuri wafanyakazi walioko chini yake na kusababisha kuchanganya maiti.

Pia, Profesa Museru ametengua uteuzi wa Mkuu wa Kitengo cha kuhifadhi  maiti,  Dk Innocent Mosha na kuwaondoa katika chumba cha maiti  wahudumu waliohusika katika matukio hayo kuanzia jana ili kupisha uchunguzi.

Katika taarifa yake kwa umma jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha alisema utenguzi wa Dk Ogweyo umetokana na kushidwa kusimamia vizuri wafanyakazi walioko chini yake  na kusababisha kitengo cha kuhifadhi maiti cha MNH kuzichanganya wakati wa kuzitoa kwa ndugu.

Alisema  jambo hilo limejitokeza mara mbili kwa kipindi kisichozidi  miezi mitatu, ambapo maiti zilichanganywa wakati wa kuzitoa kwa ndugu hali iliyosababisha usumbufu kwa wafiwa na hospitali pia.

Itakumbukwa kuwa Aprili 9, mwaka huu tukio kama hilo lilitokea na kusababisha usumbufu kwa ndugu.

“Tukio hilo limejitokeza tena Juni 20, 2016.”

“Katika uchunguzi huu, kamati maalumu, imeundwa kuchunguza kwa kina utendaji wa kitengo cha kuhifadhi maiti ili kutoa mapendekezo ya jinsi ya kurekebisha utendaji wa kitengo hicho ili matukio kama haya yasijitokeze tena,”alisema Aligaesha.

 Kutokana na utenguzi huo, Profesa Museru amemteua Mkuu wa Idara ya Radiolojia,  Dk Flora Lwakatare kukaimu nafasi hiyo na Dk Herbert Nguvumali kukaimu nafasi, mkuu wa kitengo cha kuhifadhi maiti.

Aligaesha alisema kurugenzi ya tiba shirikishi inasimamia Idara ya mionzi na Idara ya maabara kitengo cha kuhifadhi maiti kipo chini ya maabara
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top