Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA YAPATA MWENEZI MPYA TAIFA.... AFUNGUKA JUU YA UTEUZI HUOTAARIFA .

Awali napenda kumshukuru mungu kwa Uhai na Kunipa neema nyingi katika Maisha yangu na Familia Yangu.

Pili niwashukuru kwa dhati Viongozi wangu wa chama Kwa imani Kubwa walionayo juu yangu na kuona Yafaa Kuniteua Kuwa Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itifaki wa CHADEMA Taifa chini ya Kurugenzi ya Uenezi ,itifaki ,mawasiliano na Mambo ya Nje .Viongozi wangu Mkt Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Vicent Mashinji nikiwa chini ya Mkurugenzi wangu Brother John Mrema wana imani kubwa hivyo  kuanzia Tarehe 01/07/2016 kupewa majukumu haya ya kuieneza falsafa , Itikadi na ilani  ya Chama kuelekea ukombozi wa nchi yetu 2020,Kihistoria nafasi hii imewahi kuhudumiwa na Mbunge Kamanda John Mnyika na sasa Naibu katibu Mkuu bara  na Mbunge Mwita Waitara .

Ni imani yangu imani huzaa imani ,naamini ninapata ushirikiano wa kutosha wa viongozi wa chama , wahudumu wenzangu wa chama ,wanachama na Watanzania kwa ujumla katika majukumu yangu haya ya kuijenga demokrasia katika nchi yetu . Nafasi hii ni changamoto mpya katika career yangu ,nafasi ambayo wanachama wenzangu wanataraji kuona matokeo ,naipokea kwa Imani ya kuleta mabadiliko chanya kwa Chama changu na nchi yangu kwa ujumla .

Mwisho niombe ushirikiano kwa kila mwanachama ,watanzania hasa vijana wenzangu ili tulete Mageuzi ya siasa za kisayansi na harakati za kimatokeo kwa manufaa ya Taifa letu .

Ahsanteni .
Mr. Hemed Ally
Mwenezi CHADEMA. Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top