Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ABOUD JUMBE AZIKWA ZANZIBAR

 Viongozi wa kitaifa wakishiriki katika sala ya kumwombea Ras wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, marehemu Alhaj Abood Jumbe iliyofanyika kwenye msikiti, Mwembeshauri Zanzibar Agosti 15, 2016. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais, Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein.

 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Abood Jumbe katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Migombani Zanzibar Agosti 15, 2016.

 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Ghalib Bilai wakiwa katika mazishi ya Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Abood Jumbe yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Migombani, Zanzibar Agosti 15, 2016.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Alhaj Abood Jumbe katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Migombani Zanzibar, Agosti 15, 2016.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Ghalib Bilal baada ya mazishi ya Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Abood Jumbe yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Migombani Zanzibar Agosti 15, 2016.

  Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Aboud Jumbe likiwasili nyumbani kwa marehemu Migombani, Zanzibar

 Watoto, Ndugu, jamaa na Viongozi mbali mbali wakipokea mwili wa Marehemu Mzee Aboud Jumbe mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Migombani ,Zanzibar.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ,nyumbani kwa marehemu Migombani Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akishiriki dua maalum kwenye msiba wa Mzee Aboud Jumbe nyumbani kwa marehemu Migombani , Zanzibar wengine pichani ni Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Mwanamema Shein (kushoto) kulia ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top