Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa
Kukamatwa kwa Kitambulilo ambaye ni miongoni mwa wakurugenzi 120 walioachwa na Rais John Magufuli kumekuja wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikimchunguza kutokana na tuhuma za rushwa.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alilithibitishia gazeti hili kukamatwa kwa Kitambulilo kwa tuhuma za wizi akiwa mtumishi wa umma.
Kwa mujibu wa Mutafungwa, Kitambulo alikamatwa Jumapili iliyopita na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana jana.
Hata hivyo, kamanda huyo alikataa kuzungumzia kwa undani kuhusu tuhuma zinazochunguzwa, lakini taarifa za uhakika zilieleza ni ubadhirifu wa Sh9 milioni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Uchunguzi huo umekuja wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji watumishi 11 wa halmashauri hiyo kuhusiana na ubadhirifu wa zaidi ya Sh110 milioni za uchaguzi huo.
Kamanda wa Takukuru mkoaani humo, Alex Kuhanda alilithibitishia gazeti hili kuhusiana na uchunguzi huo, lakini alikataa kuingia kwa undani akisema sheria haimruhusu kufanya hivyo.
Post a Comment