Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS! Dk. Mwaka hatimaye akamatwa



Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka, baada ya kumsaka Kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Jeshi la polisi lilikuwa likitekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe Kwa kukiuka agizo la Serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala, ambao walimkuta na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la, kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

Tabibu Mwaka anashikiliwa na polisi Kwa mahojiano katika kituo cha kati.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top