Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.
Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo Ijumaa.
Post a Comment