Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS.... UVCCM DAR WASHTUKIA MBINU CHAFU ZA CHADEMA... WATOA ONYO KALIUVCCM MKOA WA DSM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Ndg: waandishi wa habari karibuni sana kwenye mkutano wetu pia tunawashukuru kwa kuitikia wito wetu wa kuhudhuria katika mkutano huu hapa ofisini kwetu.Ahsanteni sana kwa ujio wenu.
Julai 27 mwaka huu kamati ya utekelezaji Umoja wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam
"UVCCM" imekutana na kujadili agenda kadhaa za kiutendaji na mambo mbali mbali muhimu kwa mustakabali wa jumuiya yetu pamoja na mambo mengine, kamati ya utekelezaji imeazmia maazimio kadhaa muhimu ambayo tungependa kupitia taaluma zenu, taarifa yetu ifike katika jamii ili itambue na kuelewa yaliojili katika kikao chetu.

Kwanza kabisa kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam inawapongeza kwa dhati wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kwa kumchagua kwa kishindo Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa Dk. John pombe Magufuli kwa kuchukua kijiti cha Uongozi toka kwa mtangulizi wake Mwenyekiti Mstaaf Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Uamuzi wa wajumbe kwa kumchagua kwa njia ya demokrasia Dk.Magufuli wameonyesha na kudhihirisha jinsi gani CCM inavyoweza kutii na kufuata matakwa ya Katiba yake na taratibu walizojiwekea, tofauti sana na vyama vingine vya siasa ambavyo unaona kabisa jinsi demokrasia inavyopodwa pondwa, lakini pia ukweli hasa vyama hivyo na viongozi wake hususan ukawa haviko tayari kuachia madaraka kwa kuwapisha wengine.
Hali hiyo kimuonekano na kiuhalisia tunaweza kuiita ni udhaifu , udikteta na ubabe wa Viongozi kung'ang'ania madaraka na vyeo jambo ambalo ni kinyume na mahitaji au uhalisia wa dhana ya demokrasia.

Katika Hotuba aliyoitoa Dk. Magufuri baada ya kuitathmini, kuipembua na kuitafakari imeturidhisha, imetuamsha na sasa tuko tayari kufuata yaleyote aliyotuelekeza kwa manufaa ya Chama chetu na jumuiya yetu ya Umoja wa Vijana.

Ilikua hotuba yenye mipango kazi, mikakati na namna ya kuwatumikia Wanachama pamoja na Wananchi kulingana na matakwa ya wakati wa sasa na ujao.

Sisi kama Umoja wa Vijana wachama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam tunamuhakikishia Dkt.Magufuli kwamba yote aliyoyaelekeza tumeyaelewa, tumeyafahamu na pia tumeyatafakari sasa tumejiandaa kutekeleza kwa vitendo na Ufanisi wa kiwango cha juu kabisa.

Lakini pia tunachukua fursa hii sisi UVCCM Mkoa wa Dar es salaam kupongeza hotuba ya Mwenyekiti Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambayo kwetu baada ya kuipitia na kuijadili, tumeona ni hotuba elekezi ambayo imejaa mafunzo na maelekezo muhimu yanayo kihusu chama chetu na jumuiya zake.

Dkt. Kikwete akiwa kiongozi alietokana na UVCCM hadi kufikia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameonyesha njia ametupa heshima na sasa amemaliza wajibu wake, hivyo tunamtakia maisha marefu na afya tele.
Katika Uongozi wake wa miaka kumi ameitumikia Nchi na chama chetu kwa Uzalendo, Uadilifu, Uaminifu na Ujasiri mkubwa wakati wote.Hakuona muhali kukiteta na kukipigania chama na Serikali yake popote pale.

Pia kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa dar es salaam imeziagiza ngazi za wilaya, kata, matawi kujadili hotuba ya Mwenyekiti Dkt. Magufuli ili ifanyiwe kazi kwa Vitendo na matokeo yake yaonekane kuleta mafanikio kuelekea Ushindi 2020.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa unazo taarifa za kiinterejensia kutoka ndani ya Chama ya Chama Cha CHADEMA kutokana na maamuzi ya vikao vitatu vya siri na vya faragha vilivyohudhuria na baadhi ya viongozi, vikao hivyo vilivyo fanyika maeneo ya Mbezi Beach, Madale na Mbweni kwa kuhudhuriwa na washauri wao wa ukachero na siasa kutoka ndani na nje ya nchi ambao waliotoa maelekezo ya hatari yenye lengo la kuhatarisha Usalama wa Nchi yetu.

Lakini pia walipitisha maazmio mbali mbali likiwepo azimio la kuandaa vurugu za maandamano nchi nzima pasipo kufuata sheria za Maandamano hayo, mjadala ulidumu kwa siku kadhaa kuhakikisha wanakubaliana juu ya uhaini wao walioupanga.
pamoja na mkakati wao wa maandamano ya nchi nzima pia wamekusudia kwa dhati kuvuruga kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano ambayo imekuwa gumzo ndani na nje ya nchi jambo ambalo wao wapinzani wameona ni athari kubwa kwao.

UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam tunaona kinacho fanyika na chadema ni kutaka kuwajengea imani wafuasi wao kabla hawaja dharau lika kutokana na uimara wa Serikali ya CCM iliyo chini ya Rais Dk.john Magufuli . UVCCM tunayatafsiri matamshi ya Mbowe ni sawa na tangazo la uasi na uhaini wa kisiasa dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Dhahiri inaonyesha wazi kabisa Vikao vyao ambavyo viliwashirikisha majasusi ya baadhi ya nchi za kiarabu zilizofanya Mapinduzi kwa kutumia Maandamano kama vile Misri, Libya, Algeria na kadhalika ambazo ziliwatumia vijana kuanzisha maandamano kila kona ya nchi zao na hatimae kufanya mauajiya raia na mali zao na mwisho kupindua nchi.

Sisi kama UVCCM Mkoa wa Dar es salaam hatuko tayari kuona nchi yetu inaingia katika machafuko kama hayo kwa tamaa za watu wachache.

Mwisho tunamaliza kwa kuunga mkono kauli ya Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa CCM Dk. Magufuli alieitoa tarehe 29/07/2016 alipokuwa anaongea na wananchi na Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida , Rais pamoja na mambo mengi aliyoyasema pia alisisitiza kuwa wakati wa siasa uchwara umepita sasa ni wakati wa kazi.
Aidha UVCCM Mkoa wa dar es salaam unatoa wito kwa Viongozi wote wa ngazi za wilaya , kata , tawi na mashina Yale yote yaliyoelekweza na Mhe: Magufuli yafanyiwe kazi kwa vitendo bila kumuogopa mtu, Chama kinapaswa kuisimamia Serikali na mtendaji yoyote asiyetoa Ushirikiano na Chama katika kusimamia Utekelezaji wa Ilani aweke bayana ili stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Imesomwa na
Saady Khimji
Katibu wa Uhamasishaji
Mkoa wa Dar es salaam
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top