Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HALIMA MDEE AMPONGEZA SPIKA JOB NDUGAI

Mwenyekiti Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa, BAWACHA, Mh. Halima Mdee amepongeza hatua ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, kuonesha nia ya kutafuta suluhisho baina ya wabunge wa upinzani na serikali.

Mdee amesema nia hiyo ni njema lakini azma hiyo lazima izingatie mahitaji ya pande zote mbili.
Akizungumza na Easta Africa Radio, Mh. Mdee amesema anaamini utekelezaji wake hautakuwa wa kibaguzi na upendeleo bali utaangalia zaidi pande zote mbili kwa lengo la uendeshaji bora wa shughuli za Bunge.

Ameongeza kwamba, kuwe na dhamira ya kweli kutoka kwa Spika ili kiongozi huyo akirudi wakae mezani na kambi ya upinzani na wahakikishe wanapambana pamoja katika kutetea haki za watanzania bila ubaguzi.

Kwa upande wa serikali kuhamia Dodoma mheshimiwa Mdee amesema serikali ihakikishe kwanza inatenga fedha za kutosha za kuhamia Dodoma bila kuathiri bajeti nyingine za serikali ambazo zimetengwa kwaajili ya maendeleo ya nchi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top