Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amesema halmashauri na mikoa nchini zimepiga hatua kubwa katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ikilinganishawa na miaka ya nyuma.
Akizungumza na kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio , Waziri Simbachawene amesema kwa sasa hali imeanza kuridhisha katika nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na usimamiaji wa miradi ya maendeleo, jambo ambalo linatia moyo katika utendaji wa serikali.
“Hali inaendelea vizuri na kwa kweli kama tukiendelea hivi, kusimamia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya ndani kama tulivyoanza Januari hadi sasa tutapiga hatua kubwa sana katika halimashauri zetu” Amesema Simbachawene
Waziri ameongeza kuwa kila fedha ambayo imepelekwa kwenye miradi inaonekana inatumika kama ilivyokusudiwa na tabia ya kusimamiana miradi imeonesha kwamba ndani ya muda mfupi wananchi wataanza kufurahia huduma mbalimbali zilizokuwa zimekwama kwa muda mrefu.
Aidha Waziri amesisitiza kwamba mabadiliko ya kizalendo yanayooneshwa na watendaji wa serikali kwa sasa yana dalili ya kufungua Tanzania mpya yenye watu waadilifu na taifa lenye kufuata sheria na utaratibu.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
Kwa Undani7 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment