Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JESHI LA POLISI LAMKAMATA KIJANA AKIUZA FULANA ZENYE NEMBO YA UKUTA ... LAENDELA KUPINGA MAANDAMANO YA UKUTA


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejiandaa kudhibiti maandamano ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuwa hakuna mtu na au kikundi chochote cha watu kitakachofanya maandamano siku hiyo.

“Habari ya Ukuta haipo,umeshabomoka na kama haujabomoka utabomoka, wakazi wa Dar es Salaam msiwe na hofu, fanyeni kazi na hata siku hiyo hakuna mtu atakayejitokeza barabarani kuandamana,”amesema.

Kamanda Sirro amedai kuwa siasa zinatakiwa kufanywa kwa amani na utulivu na kwamba wanasiasa wanaoitumia siasa kufanya vurugu hawatafanikiwa.

“Mimi niwahakikishie kwamba tunajiandaa kwelikweli kuhakikisha watu wanafuata sheria , anayetaka kuvunja sheria kwa kufanya maandamano aanze yeye ili nasi tuanze naye,” amesema.

Ameongeza kuwa ” Suala la utii wa sheria ni la msingi,kama kuna watu au kikundi cha watu kinataka kuitumia siasa kufanya uvunjifu wa amani wajue kwamba nafasi hiyo kwa Dar es Salaam haipo.”

Aidha,Kamanda Sirro amesema August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘
  
Amesema  Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top