Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LEMA APANDISHWA KIZIMBANI ... AACHIWA KWA DHAMANA

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti mahakamani katika kesi mbili tofauti.

Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”

Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.

Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali,  Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.

Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.Kesi hiyo itatajwa tena Septemba

Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa ni Innocent Njau.

Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema magereza kwa madai kuwa wadhamini wamechelewa, lakini mbunge huyo alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top