Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

POLISI DAR WAANZA MAZOEZI YA UKAKAMAVU

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeanza mazoezi ya ukakamavu katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke kwa lengo la kudhibiti uhalifu.

Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya mazoezi hayo, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Simon Sirro, alisema mazoezi hayo yatafanyika katika mikoa yote mitatu ya kipolisi.

Mazoezi hayo yalianza saa 1:00 asubuhi katika viwanja vya Polisi Barracks na hatimaye kwenda viwanja vya Mwembeyanga na viwanja vya Zakhem huku askari hao wakiwa na vifaa vyao vya ulinzi. Walipita katika maeneo ya Kongowe na Kigamboni.

“Lengo letu ni kuzuia uhalifu na kupambana na uhalifu hasa ‘panya road’ ambao wamekuwa wakizunguka kwenye maeneo ya Temeke. Mazoezi yetu yamekwenda vizuri na tunaamini wananchi wameona vifaa vyetu vya Jeshi la Polisi na ukakamavu wa askari wetu,” alisema.

Alisema mazoezi hayo hayalengi kuwatisha wananchi ila kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali.

Alisema wamekuwa wakifanya mazoezi hayo kipindi cha nyuma lakini sasa ndio wameamua kuwaita wanahabari.

Aidha, alisema mazoezi hayo ni endelevu na baada ya kupita katika Mkoa wa Temeke watahamia Mkoa wa Kipolisi wa Ilala na Kinondoni lengo likiwa ni kukomesha uhalifu katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top