Waziri wa Habari, Utamadhini Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amevitaka vyama vya Michezo nchini kujega Ofisi katika Uwanja wa Uhuru kwa kuwa mpaka sasa michoro kwa ajili ya majengo ndani ya Uwanja huo ipo tayari
“Kama kuna vyama vya michezo vyenye uwezo binafsi au kama wanaweza kupata ufadhili wa kuja kujenga ofisi zao humu michoro ipo tayari na eneo lipo tayari ata kesho waje wajenge ” alisema Mhe. Nape.
Mhe. Nape amesisitiza kuwa zoezi hili litaratibiwa na Serikali moja kwa moja na kutoa nafasi kwa vyama vyenye uwezo kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo ambapo ramani,michoro na eneo lipo tayari kwa ajili ya zoezi hilo.
Aidha Serikali imewaalika wadau mbalimbali kuwekeza katika michezo kwa kujenga miundombinu itakayosaidia kukuza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali na kusukuma gurudumu la maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel amevishauri vyama vya michezo nchini kuchangamkia fursa iliyotolewa na Serikali ya kujenga ofisi za vyama vyao ndani ya Uwanja wa Uhuru na kushauri wadau wa michezo kuwekeza zaidi katika michezo hasa kwa vijana.
“ Wadau kimbilieni fursa ndio hii ya kuwekeza katika michezo pamoja na vyama vya michezo kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maendeleo yao na michezo nchini” alisema Prof Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi wa Wizara na Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo 22 Agosti 2016
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
Burhan awekewa vikwazo na Marekani16 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment