Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TCRA WAJA NA KAMPENI MPYA KUDHIBITI MAKOSA YA KIMTANDAO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) James Kilaba amewataka wadau wa mawasiliano nchini kujiepusha na sheria za ukiukwaji wa mitandao kwa kutokusambaza ujumbe ulio na maudhui ya uchochezi na uzushi.

James Kilaba ameyasema hayo wakati akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam  juu ya matumizi sahihi na salama ya mitandao mbapo amesema kuwa watumiaji wa mitandao wanatakiwa kutotoa maudhui ya uchochezi pindi wanapo pokea ujumbe huo kwa mtu mwingine.

“Nina wataka mfute maramoja pindi mnapopokea taarifa za uchochezi na kutoa taarifa kwa wanaohusika mnazipokea taarifa hizo” Alisema Kilaba.

Kilaba ameongeza kuwa watuamiaji wa mitandao wasitengeneze akaunti kwa lengo la kufanya utapeli au kutumia taarifa zisizo za kwao na kusisitiza kuwa wanatakiwa kutunza vifaa wanavyohifadhia kumbukumbu zao.

Kufuatia hali hiyo TCRA wamezindua kampeni ya TZ-CERT(Tanzania Computer Emergency Response Team) kwa lengo la kuongeza ufahamu kwa watumiaji wote wa mtandao baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto kwa watumiaji wa mitandao, hivyo kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kupitia mtandao wa Facebook, Twitter.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top