Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAALIMU WOTE WAPEWA SIMU ZA IPAD MKOANI SIMIYU


MKUU WA MKOA SIMIYU AMWAGA IPAD KWA WALIMU WA SHULE MKOA WOTE.

*Mkuu wa Mkoa Simiyu Ndugu Anthony Mtaka-Akikabidhi IPAD (Vishikwambi) Kwa Wakuu wa shule zote za Msingi Mkoani Simiyu*

Jumla ya IPAD 637 zimetolewa kwa Walimu wakuu 516 na waratibu wa elimu Kata 121 kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu.

IPAD hizo zimetolewa na shirika lisilo la Kiserikali EQUIP TANZANIA zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 200 za kitanzania.

Lengo la IPAD hizo ni kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za kielimu kutoka kwenye mashule yote mkoani simiyu na zitaunganishwa na mfumo rasmi wa serikali ofisi ya Rais TAMISEMI.

 Shirika hilo pia limetoa pikipiki kwa waratibu elimu kata wote 121 mkoa wa Simiyu pamoja na posho ya shilingi laki mbili kwa mwezi kwa kila Mratibu elimu kata Mkoani Simiyu.

Mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi makubwa ya kielimu katika miaka michache ijayo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top