Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAOMBAJI WA MIKOPO YA HESBL WAPEWA TAHADHARI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwatahadharisha  waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na umma kwa imepokea taarifa kuwa kuna watu wasio waaminifu ambao si watumishi wa Bodi huwapigia simu baadhi ya waombaji kwa lengo la kuwatapeli.

Taarifa hizo za kitapeli zimekuwa zikisambazwa katika siku za hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwataka baadhi ya waombaji wa mikopo au wadhamini wao kutuma fedha (Tshs 39,000/-) kwa namba ya simu 0716463190 ili fomu zao za maombi ya mikopo zilizowasilishwa Bodi zirekebishwe kwa kuwa zimeonekana zina makosa na hivyo hawatapata mikopo.

Namba inayotumika kusambaza taarifa hiyo au kupiga simu kutoa taarifa hizo ni 0764640325 na mtu anayepiga anajitambulisha kwa jina la Charles Amos.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kuwa taarifa hizo si za kweli. Mtu huyo ni tapeli na si mtumishi wa Bodi ya Mikopo.

Iwapo waombaji watapigiwa simu na matapeli hao, watoe taarifa kwa vyombo vya dola kwa hatua zaidi.

Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kuwa utaratibu wa Bodi kuwasiliana na waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi hubainika kuwa na upungufu haujabadilika. Mara baada ya kazi ya ukaguzi wa fomu kukamilika, Bodi ya Mikopo itatoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo tovuti yake (www.heslb.go.tz) na kuwaalika waombaji kufanya marekebisho.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi iliyotajwa hapo juu.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
IJUMAA, AGOSTI 12, 2016
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top