Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATU WAWILI MBARONI KWA KUMTUSI RAIS MAGUFULI MTANDAONI

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari.


Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wakikabiliwa na tuhuma za kusambaza Ujumbe wenye kuashiria kuhatarisha amani ya nchi kupitia mtandao wa simu.

Hatua hiyo pia inayohusishwa na Tukio la Oparesheni Ukuta lililopangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) lifanyike Septemba mosi mwaka huu licha ya serikali kupinga jambo hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari,wanaoshikiliwa ni pamoja na mkazi wa kata ya Isanga jijini Mbeya Moses Mwaifunga(28) na Meshaki Mgaya(28)mkazi wa Ileje mkoani Songwe.

Kamanda Kidavashari ameonya wafuasi wa Chadema na wananchi wengine kuepuka kusambaza jumbe zinazoonekana kukiuka miiko na maadili ya Utaifa na pale wanapotumiwa kabla ya kuzituma kwa watu wengine wazifute au kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Amewataka pia wananchi kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa na mamlaka huku akisisitiza kuwa hata maandiko matakatibu katika baadhi ya vitabu vya dini yanaeleza kuwa Kila Mamlaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top