Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ZIARANI MKOANI KATAVI


MAPOKEZI makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili leo mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Katavi inayoambatana na kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya maendeleo na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa kitaifa kutembelea mkoa wa Katavi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, ziara ambayo itamfikisha pia katika mkoa jirani wa Rukwa.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi, Lauteli Kanoni amesema ziara ya Waziri Mkuu mkoani humo itaanza leo na kutarajiwa kuhitimisha ziara yake Agosti 23, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, Waziri Mkuu atawasili leo mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Mpanda kisha ataelekea Ikulu Ndogo ambako atasomewa taarifa ya mkoa na kuzungumza na watumishi wa serikali katika viwanja vya ikulu ndogo.

Siku itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha Majalila, kunakojengwa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji kijijini humo kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara.

Kwa mujibu wa ratiba yake, anatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika kijiji cha Ndui kilichopo kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba na katika uwanja wa Azimio, Manispaa ya Mpanda.

Aidha, Agosti 22, mwaka huu Waziri Mkuu atafanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa Inyonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kabla ya kuelekea katika Kijiji cha Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe atakapokagua ujenzi wa daraja la mto Kavuu na baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara.

Waziri Mkuu Majaliwa anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake Agosti 23, mwaka huu katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini Mpanda kabla ya kuelekea wilayani Nkasi kuanza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top