Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUPOKEWA RASMI DODOMA ALHAMIS HII

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa kwanza wa hadhara katika uwanja wa Jamhuri akiwa mkazi wa Mkoa wa Dodoma mara tu baada ya kupokewa rasmi mkoani hapa Alhamisi wiki hii.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini, Christina Mndeme, wakati wa mkutano wake na viongozi wa dini uliofanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki.

Alieleza kuwa, baada ya Waziri Mkuu kupokelewa katika eneo la Mtimba, msafara wake utaelekea uwanja wa Jamhuri ambapo atazungumza na wananchi wa mkoa wa Dodoma.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba viongozi wa dini, kushirikiana na serikali wilayani kumpokea waziri mkuu.

Alisema, waziri mkuu anahamia rasmi mjini hapa kwa ajili ya makazi na kuendesha shughuli zake mbalimbali, ikiwemo za chama na Serikali.

Kauli hiyo imetolewa wakati Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, ikisema ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu upo katika hatua ya mwisho kukamilika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisema hayo, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa makazi hayo.

Aidha, Mhandisi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Joseph Mhamba, alisema shughuli zote za ukarabati zinazofanywa na Wakala wa Majengo (TBA), zinaendelea vizuri. Mhamba alisema kazi itakamilika kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake, Mhandisi Kashimilu Mayunga kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma Mjini (Duwasa), alisema kazi inayoendelea ni kuchimba mitaro na kulaza mabomba. Alisema kazi hiyo imekamilika kwa zaidi ya asilimia 70 na wanachosubiri sasa ni pampu.

Meneja wa mtandao wa Shirika la Simu (TTCL), Flavian Mziray alisema kazi ya kupeleka mawasiliano makazi ya Waziri Mkuu, inakaribia kukamilika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top