Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI WA ELIMU PROF. NDALICHAKO AIGEUKIA VETA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi naTeknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya VETA kufanya tathmini ya mafunzo wanayotoa katika vyuo vyote nchini ili kuona kama yanaendana na matakwa ya serikali ya kuwa na wataalamu watakaofanya kazi kwenye viwanda.

Aliagiza hivyo alipofanya ziara katika chuo cha VETA kilichopo Kipawa, Dar es Salaam jana, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya katika vyuo hivyo ili kuona namna vinavyotekeleza majukumu.

Alisema katika vyuo ambavyo ametembelea amekuta changamoto za kuwepo kwa mashine zilizoachwa bila ukarabati kiais cha kushika kutu na nyingine nzima kutotumika wakati kukiwa na vyuo vinavyozihitaji.

“Ni vizuri kukawa na usawa wa mahitaji katika vyuo vyote vya VETA kwenye kila mkoa, kulingana na uhitaji na si vyuo vingine kuwa na vifaa na vingine kuvikosa”,alisema.

Katika hatua nyingine, Profesa Ndalichako aliitaka menejimenti ya VETA kuweka mifumo ya mapato vizuri ili fedha zinazopatikana kutokana na kazi wanazozifanya ziweze kuendeleza mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo.

Aidha, aliwataka kuhakikisha udahili wa wanafunzi unaofanyika unaendana na ukubwa wa vyuo ili kutimiza azma ya serikali kuwa na vijana wengi wanaopata ajira na kujiajiri.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Geophrey Sabuni, alisema chuo hicho cha Kipawa kinatoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), yanayolenga kuhudumia viwanda kwa teknolojia ya juu zaidi.

Alisema matokeo ya mafunzo wanayotoa yanajidhihirisha wakati wanafunzi wao wanapokwenda kwenye mafunzo ya vitendo kwa sababu wengi hupata ajira na kushindwa kurudi chuoni kumaliza mafunzo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top