Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AFIKISHWA MAHAKAMANI KUTISHIA KUMPINDUA MADARAKANI RAIS MAGUFULI KUPITIA MTANDAO WA WHATSAAP

Mfanyabiasha  Leonard Materu (31) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kutuma ujumbe wa kumtishia Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.

Materu ambaye ni mkazi wa Moshi Bar Kwadiwani, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth Bankika.

Akisoma mashitaka Wakili Diana alidai, mshitakiwa huyo amefunguliwa kesi hiyo ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa WhatsApp chini ya Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015.

Ilidaiwa kuwa, Julai 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Materu aliandika ujumbe wenye lengo la kudanganya umma kupitia WhatsApp ukisomeka; “Magu ajiandae tunaenda kupindua mpaka Ikulu.”

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kumtishia Rais John Magufuli. Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo, na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja alisaini hati ya Sh milioni tano. Kesi itatajwa tena Septemba 20, mwaka huu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top