Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS ... Mbowe atoa kauli mpya ya kuwatuliza wana Chadema juu ya UKUTA



Hon Freeman Mbowe: Makamanda Salaam!

 Nimesoma mawazo mengi mitandaoni.

Naheshimu sana hisia zenu. Nakubali kwa unyenyekevu kubeba hasira na matusi ya baadhi yenu. Kwa mliotetea uamuzi wa Chama nawashukuru sana.

Uongozi na mafanikio ya chama yanahitaji uvumilivu na unyenyekevu kwa wote, viongozi na wanachama. Ujenzi wa CHADEMA siyo tukio (event) bali ni mchakato (process).  Ni mjumuiko wa matukio na mwendelezo wa fikra chanya na mikakati endelevu (sustainable strategies) zinazolenga tunakokusudia kufika.

Siku zote ninaamini siasa ni "game of dynamics" na kamwe haiwezi kufanikiwa kwa kuwa "static in thinking and action". Wajibu mkubwa wa uongozi wa chama ni pamoja na kujua mipango ya adui na namna ya kuikabili kwa manufaa mapana ya chama na zaidi malengo yetu.

Nikiwa kama Kiongozi wa chama, wajibu wangu mkubwa ni kusoma "mchezo" wa adui na kushauriana na wenzangu njia bora za kuukabili. Hii ndiyo siri ya mafanikio yetu. Huu ndiyo utamaduni wetu... culture and lifestyle!

Faslafa yangu ya "kubadilishia gia angani"  inapobidi haina historia ya kukiumiza chama japo mara nyingi husababisha mshtuko mkubwa mwanzoni.

Nilipata bahati ya kuwa muasisi wa chama hiki. Katiba ya kwanza ya Chadema iliandikiwa ofisini kwangu.

Nimekitumikia chama kwa miaka zaidi ya 24. Kama ni maumivu nimeyapata kuliko wengi wenu mnavyoweza kufikiri. Silalamiki, kwani nilikubali na kujituma katika wajibu huu, japo napoona matusi dhidi yangu na wenzangu kwa maamuzi tuliyofanya kwa nia njema kwa chama na Taifa,  kama binadamu, naumia sana lakini siku zote nimekataa na nitaendelea kukataa kuondolewa kwenye focus ya malengo yetu!

Niwakumbushe makamanda kuwa "To retreat is not to surrender but rather a strategy of war". Safari bado ni ndefu. Tulikotoka ni mbali na tulichovuna si haba. Tuna kila haki na sababu ya kutiana moyo. Tusilie na kukimbia, tujipange zaidi na tusonge mbele.

Siasa ni "vita" ya kifikra. Vita hii lengo lake la kwanza ni kuvuta hisia za watu, ziwe chanya au hasi. (Perception). Tujiulize: tumefanikiwa katika hili? Nina imani jenerali mzuri ni yule anayeweza kushinda vita bila kupoteza askari wake.

Tuwe wakweli na kila mmoja ajiulize katika eneo lake alikuwa amejipanga vipi kuutekeleza UKUTA! Aliwapanga vipi wenzake? ... majirani, marafiki, ndugu nk

 Tunapoingia sasa kwenye "UKUTA PHASE 2", tunahitaji mshikamano na mbinu zaidi.   Tunahitaji kuiona fursa hii kwa ku-perfect October 1.

Nimalizie kwa kuwakumbusha. Tunapenda kusema "...wao na pesa na majeshi sisi tuna Mungu..." Kwa imani hii nawezaje kupuuza ushauri wa viongozi wetu wote wa Kiroho!!

Kumbukeni tulisema tangu mwanzo UKUTA siyo CHADEMA pekee bali ni wa kila Mtanzania anayependa utawala wa Kidemokrasia wenye kuongoza kwa haki, sheria na Katiba.

Tuvute subira tujenge UKUTA imara zaidi.

Freeman Mbowe (MP)
Mwenyekiti na KUB
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top