Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HUYU NDIYE MISS KINONDONI 2016

 Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward akiwa katika pozi baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar jana.

Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar jana. Kulia ni mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top