Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jarida maarufu Duniani la Forbes laanika siri nzito za ndege za Bombardier

Na Mwandishi Wetu
WAKATI Serikali ya Tanzania ikiwa imenunua ndege mbili za aina ya Bombardier Dash8 Q400 kutoka Canada, imebainika na kusisitizwa kuwa ndege hizo zina usalama mkubwa, zinatumia mafuta kidogo na kutabiriwa kuwa nguzo muhimu kwa usafiri wa bei chee wa ndani ya nchi mbalimbali.

Hayo yamo katika makala iliyoandikwa na kuchapishwa na jarida mashuhuri duniani la Forbes ikiwa na anuani “Can Bombardier’s Q400 Save Regional  Air Service in the US?” ambapo mwandishi anafafanua faida za ndege hizo ikilinganishwa na nyingine zinazofanya usafiri wa ndani Marekani.“Bombadia ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika Forbes.
Faida nyingine inayotajwa ya Bombardier ni matumizi ya mafuta. Forbes wanaandika kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutumia mafuta kidogo sana kiasi kwamba hata bei ya tiketi zake itakuwa chini na kuwasaidia abiria wengi wa ndani.“Kutumia kwake mafuta kiasi kunaifanya Bombardier kuwa na ufanisi wa asilimia kati ya 48 mpaka 50 za kuwa bora zaidi ya ndege nyingine za ukanda huu,” linaandika Forbes.
Forbes wanasisitiza kuwa kutokana na gharama za matengenezo kupanda, na gharama nyingine za uendeshaji ikiwemo mishahara mizuri kwa marubani, kuna uwezekano mkubwa kwa Bombardier kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege nyingine.
“Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina ya Bombardia ndio zitakuwa mbadala na zitashika njia nyingi za ndani (Marekani) kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa (kutokana na gharama kubwa kwa ndege nyingine) katika viwanja takribani 20,” linaandika zaidi Forbes.Akikaririwa katika makala hiyo,  Mike Arcamone, Rais wa Masuala ya Biashara wa Bombardier anasema wasiwasi wa awali wa abiria kuhusu ndege hizo kutumia mfumo wa turbo sasa umeondoka kwa kuwa injini na dizaini ya kisasa ya ndege hizo inaifanya isiwe na kelele kama ilivyodhaniwa.
“Wanunuzi wengi wa ndege hizi wamebaini kuwa hazina kelele na watumiaji wengi wanaamini kuwa zinaweza kuwa mbadala wa ndege nyingine za bei nafuu,” anasema afisa huyo kauli inayokubaliwa na wachambuzi wa Forbes.
Tayari Serikali ya Tanzania imeahidi kuleta ndege nyingine ya pili wiki hii baada ya ile ya kwanza kuwasili nchini wiki iliyopita ukiwa ni mkakati na utekelezaji wa ahadi ya Rais John Pombe Magufuli ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Kuwasili kwa ndege hizo kunaashiria mengi lakini muhimu ni uthabiti wa ahadi za Dkt. Magufuli akiwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, ambapo mambo mengi makubwa ambayo ameyaahidi ameanza kuyafanyiakazi na kuwakuna wengi nchini na nje ya nchi.Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top