Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JPM ATIMIZA AHADI YA NDEGE MPYA YA AIR TANZANIA LEO ... BEI NA SIFA ZAKE ZATAJWAHatimaye ndege moja wapo ya zile mbili zilizonunuliwa na Serikali ya awamu ya Tano inatarajiwa kutua leo saa saba (1015 UTC) ktk uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), safari ya ndege hiyo kuja nchini ilianza mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia na kutoka Ethiopia itatua Dsm ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.

Ili kuepusha muingiliano na ndege nyingine za abiria (scheduled flights) za ndani ya nchi na zile za kimataifa katika eneo la Terminal Two, ambapo mida hiyo itakuwa ndio "peak hours", ndege hiyo itakapotua itaongoza moja kwa moja eneo la Terminal One, VIP Apron kwa ajili ya kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.

Kama ilivyo utaratibu na utamaduni wa usafiri wa anga..kabla ya kuingia "apron" ndege hiyo itapata "Water Cannon Salutation" kutoka Magari ya Jeshi la Zimamoto kama ishara ya kuikaribisha kabla ya kuvuka gate kuingia eneo la maegesho. Na baadae kutakuwa na hatua za kukata utepe, hotuba na mengineyo.

Wakati ndege hii ikiingia leo, ndege ya pili ambayo tayari imekaguliwa na Maafisa wa Ukaguzi toka Mamlaka ya Anga Tanzania(TCAA), itakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania 22/09/2016 na kuanza safari ya kuja nchini Tanzania 23/09/2016.

Wakati huo huo tuendelee kufahamu undani wa ndege hizi:

BOMBARDIER DASH8 Q400

Jamii Yake Nyingine: Bombardier Dash 7/8 & Q 200/300/400.

Kutengenezwa: CANADA

SIFA ZAKE:

Abiria: (passengers) 74-90

Urefu: (Length) 32.6 mita.

Kimo: (Height) 6.40 futi.

Upana: (Width) 8 futi.

Nguvu/Injini: (HorsePower)10,142 HP

Spidi: (AirSpeed) 666.7 Km/h

Umbali Inayoenda: (Max.Range) 2522.4 km.

Umbali Kuruka Juu: (Cruising Altitude) 27,000 futi.

Uzito Wa Kubeba: (Max Payload) 8.7 tani.

Full Tank: (Fuel Capacity) 6617 lita.

Mda Inayotumia Kufika Umbali wa Juu: (Time to Cruising Altitude)18 dak.

Urefu Njia ya kurukia: 1067mita

Urefu Njia ya Kutua : 1286mita 

Ulaji Mafuta: (Fuel Economy/Km) 16,940/-Tzs kila 1.8 km.

Bei kwa Ndege Moja: (Price range) 
66 bilioni.

Karibu nyumbani Bombardier Dash 8 - Q400
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top