Loading...
Lowassa aipongeza Serikali utaratibu maafa ya tetemeko la ardhi
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leoofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake
Na Mwandishi Wetu-KAGERAWaziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.
Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.
“Napenda nikupongenze mkuu wa mkoakwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwahiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.
Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa sualahili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.
“Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema Meja Generali Salum Kijuu.
Post a Comment