Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKUBWA FELLA AANIKA HADHARANI NYUMBA ALIZOWAJENGEA YAMOTO BAND

 Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.
 Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
 Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima

MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band na kuwataka wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji nyumba na sio magari.

Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza kuwazawadia nyumba wasanii wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi hasa baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.

Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka sasa hajajua thamani yake ila zitakapokamilika ataita watu wa tathmini kwa ajili ya kuziangalia ili kujua zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.

Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.

Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii wenyewe wanazozipata kwenye shoo za muziki wanazozifanya na sio kama hela zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na hatua hii kwani ni mara chache sana kwa viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo na amewataka wasanii kutokufanya mzaha kwenye tasnia hii.

Fella amezindua pia nguo aina mbalimbali zenye nembo y Yamoto Band na wamezilipia Brela,COSOTA kwa hiyo yoyote atakayejaribu kunakili watamshughulikia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top