Loading...
Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Bandari ... Atoa maagizo mazito
Ameingia ukumbini saa 6 mchana huu. Amesubiriwa sana na wafanyakazi watoe kilio chao
Anasikitishwa na vyeti feki feki. Mtu amesoma hadi darasa la saba lakini CV yake inaoneshwa ana degree mbili. Kasema sasa ni wakati wa Mtu Kufanya kazi kulingana na Elimu yake. Amesema hawa wa juu waliofoji vyeti atalala nao mbele. kama umefoji vyeti jisalimishe mapema.
Ameshangaa kukuta Scanner za kukagua mizigo hazifanyi kazi. Ameagiza TPA, TRA Wizara ya Uchukuzi wakae leo kikao kuhakikisha zinaongezwa scanner ndani ya miezi mitano zifike scanner sita. Na hizi zilizopo zifanye kazi. Anahitaji hiyo report leo hata wamalize saa nane usiku.
Kazungumzia Uozo wa Bandarini kataka Ukomeshwe. Anataka watu wajitume kufanya kazi.
Meli zaidi ya 60 zilikuwa zinapita bila kulipiwa kodi, bora ipite meli moja ilipie Kodi kuliko kujaza Mameli bandarini yasiyolipa kodi.
Mkataba wa TICTS ilikuwa wa miaka 10 lakini ukaongezwa Kinyemela miaka mingine 15 hivyo kaagiza TPA na TRA wapitie upya Mkataba huo.
Kaagiza TPA, TRA na USalama/Polisi washirikiane kwenye kuendesha Scanner. Sio kila kitengo kiwe na Scanner yake Matokeo yake report zinakuwa tofauti. Hivyo kata scanner awepo mtu wa Badari, Polisi, na TRA.
Ziara yake ilianzia kule Kurasini oil jetty Berth 12.
Post a Comment