Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ushetu yapata tuzo ya Halmashauri bora

HALMASHAURI ya wilaya ya Ushetu imeshinda Tuzo za Halmashauri Bora (Mayors Award) inayotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT).

Ushetu ambayo iko katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga ilizawadiwa trekta lenye thamani ya Sh milioni 56 baada ya kutangazwa mshindi wa jumla wa tuzo hizo mjini Musoma juzi usiku.

Trekta hiyo imenunulia kwa ufadhili wa benki ya NMB ambayo pia imefadhili kwa kiasi kikubwa mkutano mkuu wa 32 wa ALAT uliofanyika Musoma kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi wiki hii.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa alikabidhi trekta hiyo mpya kwa viongozi wa Ushetu kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene. Mbali na kuibuka mshindi wa jumla halmashauri hiyo ya Ushetu ilipata tuzo katika eneo la utoaji wa huduma bora na utawala bora.

Halmashauri nyingine zilizopata tuzo katika maeneo mbalimbali ni Tanga, Mbeya, Shinyanga, Arusha, Iringa, Tabora, Njombe na Masasi.

Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu na Utafiti wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Ichikael Maro alipewe fursa ya kukabidhi tuzo kwa halmashauri zilizofanya vizuri kwa upande wa huduma (service delivery).

Halmashauri hizo ni Ushetu, Iringa na Tanga kwa upande wa majiji. Kampuni ya TSN ni miongoni mwa wadau waliofadhili mkutano huo mkuu wa ALAT ambao umemalizika jana.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top