Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vyeti feki TPA; Wafanyakazi 600 kuachishwa kaziZaidi ya wafanyakazi 600 wataachishwa/kufukuzwa kazi kutokana na kuwa na vyeti feki/kughushi vyeti vya kitaaluma.

Hiyo imegundulika kutokana na zoezi la uhakiki linaloendelea katika taasisi hiyo ya Mamlaka ya Bandari -TPA.Zoezi la uhakiki linaendeshwa na NECTA.

Mpaka sasa majina ya wafanyakazi wenye vyeti feki wapatao mia tatu(300) yameshapatikana na wahusika kutakiwa kumwona afisa mwajiri kwa maelekezo zaidi.

Habari za uhakika zinadokeza kuwa kufikia tarehe 26 Mwezi September majina mengine zaidi ya 300 yatakuwa yamethibishwa kuwa ni ya wafanyakazi wenye vyeti feki.

Hii itafanya idadi ya walioghushi vyeti kufikia 600 katika Mamlaka hii yenye neema kwa mishahara mizuri na marupurupu yanayovutia.

Katika kila kinachoshangaza wengi wengi wenye vyeti feki ni wale wanaoshika nafasi mbalimbali za uongozi(senior officers).

Habari hii pia inapatikana kwa kirefu katika gazeti la The Guardian tolea la leo.

Nimetimiza wajibu wa kutoa na kupokea taarifa kwa maslahi mapana ya Tanzania ya viwanda.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top