Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya kiasi cha shilingi 154 milion zimetolewa kwa Waalimu 701 wa shule za msingi na sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa kulipa posho za nauli na simu za madiwani wa jiji la Arusha.
Akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini hapa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Gabriel Daqqaro alisema kuwa kutokana na malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho waliokuwa wanadai walimu kwa kipindi cha mda mrefu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanya kazi ya kufundisha watoto wetu kwa moyo.
Daqqaro alisema kuwa baada ya kikao na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la Arusha, na kuagizwa kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki mbili na agizo hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao zote walizokuwa wanadai.
Alisema kuwa fedha zilizolipwa waalimu hao tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani posho za usafiri na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya waalimu na mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung'unuko kutoka kwa waalimu.
''Hapa napenda tusiingize ushabiki wa kisiasa katika hili na tuache kuzusha maneno maneno yanayaashiria uvunjifu wa amani maana tayari nimeshaanza kusikia maneno maneno yanazuka kutoka kwa madiwani, sasa nasema hivi, sisi tumeamua kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa ,na kunakili madiwani wanadai kuwa wao walikuta fedha hizi zikilipwa na ndio maana wakaendelea kupokea,hivyo nnachotaka kuesma kama kweli walikuwa na nia njema na wananchi kwanini wasizikate mapema mpaka wasubiri mkuu wa mkoa aje aone mambo hay,na wao ndio waanze kuongea maneno maneno''alisema DC Daqqaro.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa wakati na kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu kupewa stahiki zao kwa wakati.
Akawataka waalimu hao kuhakikisha malengo ya mkoa kuongeza ufaulu yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa moyo mmoja huku serikali ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa huo.
Malipo hayo ya waalimu 701 yametokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka DC na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu walioyatoa kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .
Post a Comment