Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mkuu Majaliwa azindua mpango mpya wa makazi

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bango lenye anwani na Postikodi ya makazi yake ya Dodoma baada ya kuzindua  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi  kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza wakati alipozindua  Miongozo ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi  kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016.

 Msanii, Mrisho Mpoto akitumbuiza katika uzinduzi wa  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakakala ya kitabu cha Miongozo ya  ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi bada ya kuuzindua kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa  amezindua miongozo ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi  na kuziagiza taasisi za umma na binafsi zianze kutumia mfumo huo ili kuchochea kasi ya maendeleo nchini. 
“Nawaagiza na BRELA (Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara) kuhakikisha wanajumuisha anauani za makazi kwa waombaji wa leseni za biashara ili kurahisisha utambuzi na uhakiki,” amesema. 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, 14 Septemba, 2016), wakati akizindua miongozo ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.   
Amesema mfumo huo lazima uweke msukumo mpya wa kimkakati ili kuhakikisha uwekaji wa miundombinu ya Anwani za Makazi na Postikodi unatekelezwa ipasavyo na unachangia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 
Amesema mfumo huo unatakiwa ukamilike nchi nzima kabla ama ifikapo Juni, 2018 ila kasi ya utekelezaji wake inakwamishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha na barabara au mitaa mingi kutokuwa na majina. 
“Hivyo, naelekeza kila mdau atimize wajibu wake katika utekelezaji na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kulingana na maelekezo yaliyo kwenye miongozo hii,” amesisitiza. 
Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tano inapenda watendaji wake kuwa wabunifu, hivyochangamoto hizo zitatuliwe haraka na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. 
Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuzitafutia ufumbuzi  changamoto ambazo hazihitaji fedha ama gharama kubwa kama kuhakikisha barabara na mitaa yote inakuwa na majina yaliyorasimishwa na kudhibiti mipango miji dhaifu na ujenzi holela. 
Amesema Halmashauri zinatakiwa kuwa na takwimu za idadi ya barabara na mitaa na nyumba katika kila katana kuwa na taarifa za wakazi wa kila kata, kujenga uelewa na uwezo wa mfumo kwa wadau na wananchina kuimarisha matumizi ya daftari la wakazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top