Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS ... Mbowe abwagwa Mahakamani .... Ashindwa kesi na NHC sakata la deni la Billicanas

Freeman Mbowe Mfanyabiashara, Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa katika picha ya maktaba.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.

Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa  kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia Ulikuwepo lakini kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.
https://3.bp.blogspot.com/-iJzwh8Zkl3U/WAXiB5W2C-I/AAAAAAAJHtA/06FFWxvoBiQfGpgj1BEmKk5LB6iyfnrZQCLcB/s640/unnamed.jpg
Mawakili wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani ) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top