Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DC Polepole apambana na viongozi wa CCM

Dar es Salaam.  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey Polepole amewapiga marufuku wajumbe wa mashina na viongozi wengine wa  CCM kujihusisha na uidhinishaji  mauzo ya ardhi, huku akiwataka wananchi kuwa makini na kufuata utaratibu wa kisheria wakati wa ununuzi.

Polepole alitoa onyo hilo jana wakati wa mkutano na wakazi wa King’azi Juu, Kata ya Kwembe, baada ya kuelezwa kuwa wana matatizo mengi ya ardhi yanayotokana na baadhi viongozi kuuza eneo kwa mtu zaidi ya mmoja.

Wananchi hao walimweleza kuwa, udanganyifu unaofanyika unatokana na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa na wajumbe wa mashina wa CCM kula njama na wamiliki wa maeneo, kuuzia watu eneo moja zaidi ya mara moja.

Polepole alisema CCM ipo kwenye harakati za kujijenga, hivyo lazima kumaliza migogoro hiyo kama sehemu ya kujirekebisha. Mwenyekiti wa mtaa huo, Seleman Bheho alisema mwaka 2014/15 alipoingia madarakani .ofisi yake ilikuwa akipata kesi za za ardhi nane mpaka 10 kwa siku, lakini sasa zimepungua hadi tatu kwa wiki.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top