Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Diwani wa Chadema anaswa na Madawa ya Kulevya, Bunduki


Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.

Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.

“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.

Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.

“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.

Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top