Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JPM 2, JK 25

Dar es Salaam. Hatua ya Rais John Magufuli kutoshabikia safari za nje kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete imeelezwa na wachambuzi wa masuala ya siasa kuwa ni kutokana na tofauti za vipaumbele vyao.

Kwa mujibu wa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, Rais Magufuli anaonekana kutoa kipaumbele kwa mambo ya ndani ya nchi kwa maana ya kurejesha uwajibikaji kwa masuala ya Serikali, utawala bora na mambo yanayofanana na hayo, wakati Kikwete alijikita kuitangaza nchi nyanja za kimataifa.

“Hili la mwingine kuonekana kuwa alisafiri zaidi na mwingine akijikita katika masuala ya ndani naweza kusema halina madhara, kwani vipaumbele vyao vinatofautiana wakati huyu anaonekana kutoa kipaumbele kwa masuala ya ndani ya nchi, kurejesha uwajibikaji kwa masuala ya Serikali, utawala bora, huyu mwingine aliamua kuitangaza nchi kimataifa jambo ambalo lilikuwa jema kwa wakati ule,” alisema Dk Banna.

Mpaka sasa Rais Magufuli akiwa anaelekea kukamilisha mwaka mmoja tangu aingie madarakani kutokana na ushindi aliopata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015, amesafiri nje mara mbili tu ikilinganishwa na mtangulizi wake aliyesafiri takriban mara 25 kwa kipindi kama hiki.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top