Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Madiwani 12 wa UKAWA wajisalimisha CCM


madiwani 12 kati ya 20 wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika Halimashauri ya Jiji la Tanga, Jana wamekubali yaishe na kuanza rasmi kushiriki vikao vya baraza la madiwani la halimashauri yao baada ya mgomo wao wa tangu mwezi desemba mwaka jana waliokuwa wakisusia vikao kushinikiza kumkataa Mstahiki meya wa Jiji hilo bwana Mustafa Selebosi wa chama cha Mapinduzi CCM, na hivyo kutafsirika kama wamejisalimisha CCM.

katika kipindi chote hicho madiwani hao walichoonyesha msimamo huo, walikuwa hawaingii katika vikao hivyo katika kutekeleza kutokumtambua meya huyo.

Madiwani hao wamekiri kumaliza tofauti iliyokuwepo sanjari na kufanya uchaguzi wa kuunda kamati za Halmashauri hiyo.
Kikao cha jana ni muendelezo wa kikao cha tarehe 19 Desemba mwaka jana ambapo vurugu zilianza baada ya Mkurugenzi wa jiji kutangaza nafasi ya umeya kuchukuliwa na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo Chama cha Wananchi CUF hakikuridhika na matokeo hayo.

 Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Mustafa Selebosi.

Akifungua kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Mstahiki Meya wa jiji la TangaMustafa Selebosi amesema wameamua kuondoa tofauti zao na kuungana kwa pamoja ili waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua sambamba na kufanya kazi za Halmashauri kwa pamoja ili kuliletea Jiji la Tanga maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la TangaDaudi Mayeji aliwashukuru madiwani hao kwa kuamua kwa moyo mmoja kufanya kazi ya kuungana kwa pamoja ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua katika maeneo yao.

Mayeji alisema kwa muda mrefu swala hilo limekuwa likiwapa wakati mgumu kutokana na vikao vya baraza kutokaliwa na kueleza kuwa viongozi wa serikali na vyama wamefanya kazi kubwa na nzuri ya kuwaunganisha madiwani hao sanjari na kumaliza tofauti hiyo.

Naye Mbunge wa jiji la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Mussa Mbaruku amesema madiwani ni jicho la Serikali katika Halmashauri hivyo wanapaswa kutambua wajibu wao ili penye hitilafu warekebishane na kuwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa nafasi aliyonayo ili Halmashauri iweze kupiga hatua
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top