Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Prof. Lipumba ateua Wakurugenzi wapya

Licha ya baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Wananchi (CUF) na wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutamka kutomtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti wa CUF, Lipumba ameendelea kufanya shughuli za chama hicho ambapo jana ameteua wakurugenzi wapya kwa madai ya kujaza nafasi za wakurugenzi alizotengua teuzi zao juzi.

Miongoni mwa Wakurugenzi aliodai Lipumba kuwateua ni pamoja na;
  1.  Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha -Thomas Malima
  2. Maftaha Nachuma - Mkurugenzi wa Mambo wa Nje CUF
  3.  Zaynab Mndolwa -Mkurugenzi wa Haki za Binadamu
  4. Jaffari Mneke -Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi.
Hata hivyo, Lipumba amedai kuwa, aliowateua watakaimu nyadhifa hizo hadi watakapothibitishwa  na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la CUF.

Aidha, amedai kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje atamteua kutoka Zanzibar hapo baadae.

Sambamba na hilo, alisema wakurugenzi na manaibu wakurugenzi aliowateua baada ya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Juni, 21, 2014 wataendelea na nyadhifa zao huku akitishia kuwa, ikimbidi kufanya mabadiliko ya wakurugenzi hao hatosita kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, Lipumba alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF ambaye ndiye Katibu wa Bodi ya Wadhamini kuitisha kikao cha bodi hiyo Oktoba 4,2016 ili ipewe taarifa ya msimamo na ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kuhusu mgogoro wa uongozi kitaifa wa CUF.

Lipumba alisema kuwa, amefanya teuzi za wakurugenzi hao kwa mujibu wa katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la 2014 ibara ya 90 (1) (f) ambayo inasema kuwa Mwwenyekiti Taifa atateua Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa au wanachama jasiri wa chama.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top