Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli anazikumbatia pesa?



Tangu Rais Magufuli aingie madarakani ametilia mkazo mno suala la ukusanyaji kodi na kuziba mianya ya upotevu wa kodi hadi kufikia hatua pesa za kiujanja janja kupotea mitaani na pesa zote kufika Serikalini moja kwa moja.

Kitendo cha pesa kwenda Serikalini moja kwa moja na kupotea mitaani baadhi ya Watu wamekuwa wakihoji Rais Magufuli kukumbatia pesa zote bila ya Wananchi kunufaika. Hiyo ni hoja nyepesi endapo utatazama majukumu ya Serikali na kipi ambacho Serikali imeshakifanya mpaka sasa.

Twende pamoja, Serikali ya JPM imetekeleza ahadi ya kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya Msingi mpaka kidato cha nne ambapo mabilioni ya pesa yamekuwa yakitumika kutoa elimu bure. Watoto wetu (Mimi, wewe na yule) wamekuwa sehemu ya kunufaika na elimu bure pamoja na kukalia madawati mapya na si tena kukaa sakafuni. Hayo ndio tu manufaa ya kodi zinazokusanywa na baadhi ya watu kusema JPM anakumbatia pesa.

Serikali ya Rais Magufuli inajenga barabara (zikiwemo za flyovers zilizoanza kujengwa), madaraja pamoja na kununua vivuko ambavyo vinatusaidia sisi wananchi kwenye usafiri na usafirishaji wa mizigo. Ujenzi huu wa miundombinu umekuwa ukitumia mabilioni ya pesa ambazo JPM amekuwa akizikusanya kupitia kodi.

Serikali ya JPM imenunua ndege 2 mpya ambapo mabilioni ya pesa zimetumika kununua ndege hizo ambazo zitakuwa mkombozi wa usafiri wa anga kwa bei nafuu na makusanyo ya kodi yataelekezwa kutoa huduma kwa jamii. Hapa kuanzia matajiri mpaka maskini watakuwa wanufaika wa ndege hizi.

Sio tu ndege bali hata upande wa usafiri wa reli umeimarishwa ambapo Serikali ya Magufuli imenunua vichwa na mabehewa ya treni mapya kabisa na hivyo kufufua usafiri wa treni ya kati ya Dar - Kigoma ambao ni kimbilio kwa watu wa kipato cha kati na cha chini. Tutasemaje hatunufaiki na makusanyo ya kodi zinazoenda Serikalini?

JPM amekuwa akilipa mishahara ya watumishi wa umma pamoja na kutoa pesa za uendeshaji wa shughuli za kiserikali. Mishahara hiyo inayolipwa kwa watumishi ndiyo inayowasaidia wafanyakazi hao na familia kuendesha maisha. Tutasemaje pesa hatuzioni wakati mishahara inalipwa?

Serikali imeendelea na ulipaji wa madeni ya ndani na nje. BoT imeanza kulipa madeni yote ya ndani na nje kwa fedha zake za ndani ambapo tayari imeshalipa kiasi cha Sh bilioni 96 za deni la ndani huku ikilipa dola za Kimarekani milioni 90 (sawa na Sh bilioni 190) za deni lake la nje.

Serikali hii inatumia mabilioni ya pesa kununua madawa, mashine, vitanda na vifaa tiba kwenye mahospitali ambapo leo hii suala la huduma za kiafya zimekuwa bora zaidi. Tutasemaje kodi inayokusanywa na Serikali haina manufaa kwa Wananchi?

Ndugu zangu, tumeona baadhi tu ya mifano ya Mabilioni ya pesa yanavyotumika na Serikali, tutasemaje JPM anakumbatia pesa?

Shilatu E.J
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top