Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UVCCM wapigilia msumari Sakata la Waalimu kumpiga Mwanafunzi



Kumb.Na.VMM/U.80/8/68.   6-10-2016




*TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA C.C.M KWA VYOMBO VYA HABARI KULAANI KITENDO CHA WALIMU KUPIGA KINYAMA MWANAFUNZI HUKO  MBEYA.*

Umoja wa  vijana wa chama cha mapinduzi Tanzania umepokea kwa mstuko taarifa ya mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ya kutwa ya 'mbeya Day'  ndg Sebastian  Chinguku wa kidato cha Tatu kupigwa kwa kuchangiwa na Walimu tarajali watatu ambao ni Frank Msigwa,John Deo na Sanke Gwamaka kwa kosa la mwanafunzi huyo kutofanya Zoezi la Darasani.

Kitendo kilichofanywa ns Walimu tarajali hawa ni cha kinyama na hakipaswi kuachwa na kufumbiwa macho.
Kitendo hiki hakivumiliki na ni kinyume na haki za binadamu na hata Sheria za nchi.

Ikumbukwe kuwa kada ya Ualimu inaongozwa na Miiko na maadili yake na sheria za nchi zipo wazi hata zinataja wazi Idadi ya viboko anavyopaswa kuchapwa mwanafunzi na sehemu husika. Rejea *"sheria ya Adhabu ya viboko namba 12 ya mwaka 1998"*
*"The corporal punishment act no,12 of 1998"*
Kwa hali hiyo basi Umoja wa Vijana wa CCM tunalaani vikali adhabu hiyo na aina za adhabu kama hizo zinazotolewa kiholela kwa wanafunzi kote nchini.

Kilichotokea Mbeya ni mwendelezo wa manyanyaso makubwa wanayoyapata wanafunzi kote nchini,Kumpiga kinyama hivyo mwanafunzi si tu kwamba kunamuumiza bali kuna athari kubwa kisaikolojia inamfanya mwathirika kutoipenda tena Shule.

*Uvccm* tunataka walimu wazingatie kanuni na taratibu za kazi.
Ukirejea kwenye kitabu cha *"kiongozi cha mkuu wa shule"*

  Kimeainisha namna ambayo mwanafunzi mtukutu anapaswa kutendewa.kuna kipengele kinazungumzia makosa yanayoweza kumfukuzisha shule mwanafunzi.
Niwasihi walimu wazingatie hilo.

Tunashangaa sana uongozi wa Shule ya sekondari  'Mbeya day' kutokujua kinachoendelea mpk leo. Tunajiuliza aina ya malezi ya walimu wa shule hii akiwemo mkuu wa Shule. Tunazidi kujiuliza Kitabu cha Mwalimu wa zamu(duty book) kinachojazwa kila siku wameshindwaje kubaini huyu mwanafunzi hayupo Shule?au kama ni mgonjwa tuna wasiwasi  Mkuu wa shule alilijua hili mapema.

Mwisho tunaitaka Serikali kupitia Waziri  wa Elimu sayansi na Teknolojia kuwafukuza mara moja walimu hawa tarajali  kwenye taaluma ya Ualimu kwa kuwafutia udahili wao mara moja. Isiishie hapo tu bali Jeshi la polisi liwatafute wahusika wote kokote kule waliko na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria mara moja.

 hawa hakika wanafaa kuwa mabondia na sio walimu.

Sasa ni wakati sahihi wa Wizara ya Elimu sayansi ns Teknolojia kusimamia miongozo na wajibu wake pasipo kusubiri mpk matukio kama haya kutokea.

Pia Uvccm tunashangazwa na Ukimya wa taasisi za kutetea haki za binadamu kukaa kimya katika kitendo hiki cha Kidhalimu.

Pole sana SEBASTIAN CHINGUKU Kwa matatizo haya .

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Imetolewa na :
*MTEMI SYLVESTER YAREDI.(Mwl)*
*KAIMU MKUU IDARA UHAMASISHAJI SERA,UTAFITI NA MAWASILIANO UVCCM TAIFA.*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top