Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Viongozi Kinondoni wakalia kuti kavu

Dar es Salaam. Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini imemuomba Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mussa Iyombe kuwachukulia hatua maofisa wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni waliohusika katika ubadhirifu wa Sh3.3 bilioni za ujenzi wa Barabara ya Masjid-Quba, Sinza jijini hapa.

Fedha hizo zilitolewa katika mwaka wa fedha 2013/14,  hivyo halmashauri hiyo kuingia mkataba wa miezi mitatu na mkandarasi ili barabara hiyo yenye urefu wa kilomita mbili iwe imekamilika.

Hata hivyo, mradi huo ulianza kutekelezwa Machi 2015 na kutakiwa kukamilika Juni mwaka huohuo lakini mpaka Juni mwaka huu ni mita 700 zilizokamilika.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Joseph Haule alisema ukaguzi wao ulibaini kuwa hata mita 700 zilizojengwa zipo chini ya kiwango.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli aliliambia gazeti hili kuwa tayari wahusika wakiwamo wahandisi na mkurugenzi wameshachukuliwa hatua za nidhamu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top