Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waalimu wanafunzi waliompiga Mwanafunzi Mbeya wazidi kushughulikiwa ... Safari hii HESLB yawashushia rungu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.
 
Na.
 
Jina
 
Chuo Anachosoma
 
1.
 
Frank Msigwa
 
Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
 
2.
 
John Deo
 
Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
 
3.
 
Evance Sanga
 
Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
 
4.
 
Sante Gwamaka
 
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwahiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo. Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingagatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.

Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top