Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ahadi ya Rais Magufuli yaanza kutekelezwa mara mojaWaziri wa ulinzi Dr. Hussein Mwinyi akiambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Lameck Nchemba Pamoja na baadhi ya wakuu wa vyombo vya Ulinzi na usalama;

Amesema serikali itaanza kulipa posho maalumu(package) kama ilivyoahidiwa na Mh. Rais kwa Askari wote wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama yani Jwtz,  polisi,  Magereza, Uhamiaji na Zimamoto kuanzia mwezi November mwaka huu kupitia mishahara yao ya mwisho wa mwezi huu,  posho hiyo ni badala ya Vinywaji vya motisha pamoja na free duty shops pia ameeleza kuwa posho hiyo italipwa pamoja na malimbikizo yake yote kuanzia mwezi Julai 2016 ilipoanza kutolewa.

 Mwinyi ameyasema hayo akiwa kwenye mkutano maalum wa vyombo vya ulinzi na Usalama mjini Dodoma. Amesema kuwa mpaka muda huu serikali imeshamaliza hatua zote za ulipwaji wa posho hiyo kinachosubiliwa ni muda wa malipo hayo kufika.

 Aidha Waziri Mwinyi amewataka askari wote kuwa wavumilivu na kuendelea kutunza nidhamu pamoja na kuzidi kuchapa kazi ya nchi kama ilivyo ada na kuwahakikishia kuwa malipo hayo yataingia mwezi huu. Akiongea kwa utani huku akicheka amesema askari msilewe sana siku hiyo mkasahau majukumu yenu juu wa Ulinzi wa Taifa letu na kuongeza kwa kusema najua mmechoka sana kuisubili hiyo pesa baada ya vuguvugu la uzushi juu ya pesa hiyo kupita lakini niwahakikishieni kuwa kila kitu kipo sawa hazina wameshamaliza zoezi lote hivyo tuwe wavumilivu tu kama ilivyo desturi yetu.

  Mwinyi ameyaongea hayo ikiwa ni sehemu ya kuwahimiza na kuwatia moyo walinzi wetu kwamba wazidi kupiga kazi kama ambavyo kauli mbiu ya serikali yetu ilivyo ya HAPA KAZI TU na kwamba Rais wetu anatujali na kututhamini sana kwa kila hali na yuko bega kwa bega nasisi tusimwangushe.

Imetolewa na
Katibu wa Waziri.
03/11/2016.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top